TAMADUNI TANO ZA KUSHANGAZA BARANI AFRICA
Photo by Abel Kayode from Pexels
Barani Afrika kuna mila, desturi na tamaduni mbalimbali ambazo kwa jamii husika ni kawaida ila zinapowafikia watu wa jamii nyingine huonekana za kustaajabisha na kutisha. Hapa tumekuchambulia tamaduni tano ambazo zitakuacha kinywa wazi.
3.Kulala na shangazi wa bibi harusi kabla ya ndoa katika kabila la Banyankole huko Uganda.
Hapa wakati vijana wanapokua wanaingia katika maisha ya ndoa lazima wachunguzwe kama wa kike ni bikra na wakiume apimwe kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa(rijali). Maajabu yanakuja katika zoezi hili ambapo shangazi upande wa bibi harusi hutumika kama kipimo. Shangazi huyo anatakiwa kumkagua Bibi harusi kama ni bikra na inapofikia suala zima la kumpima bwana harusi shangazi anatakiwa alale nae (kufanya tendo la ndoa) kuhakikisha kwamba bwana harusi anamudu tendo la ndoa na kuhakikisha kwamba binti yao anapata mwanaume rijali. Zoezi hili hufanyika kabla maharusi hawajalala pamoja.
Wakati mwingine shangazi huhitajika kuhakiki suala hilo kwa kwenda kushuhudia mubashara maharusi wakifanya tendo la ndoa.
4. Kuchapwa mijeledi ili upewe mke na heshima kubwa.
Katika jamii ya wafulani huko Benin kupata mke sio jambo rahisi hasa pale upande wa bibi harusi wanapochagua mahari ijulikanayo kama 'sharo' ambapo bwana harusi anahitajika kuvumilia kichapo cha mijeledi kutoka kwa wazee wa upande wa bi harusi ili kupewa mke na heshima. Wakati wa zoezi hili kama bwana harusi atashindwa kuvumilia mijeledi basi ndoa hiyo huwa batili.
5. Kitambi kikubwa ndio sifa ya kupata mke.
Kabla ya sherehe za kupata mke katika mwezi wa sita na wa saba katika bonde la Omo huko Ethiopia, mwenye kitambi kikubwa ndio anapewa kipaumbele katika kupewa mke.
Kabla ya sherehe hizi vijana ambao bado hawajaoa hupewa muda wa kujiandaa kwa kujitenga porini ambapo huko wanakunywa damu ya ng'ombe na maziwa kuweka afya safi. Siku ya mashindano kila familia yenye kijana ambae hajaoa humleta ili kulinganishwa na wengine. Mwenye tumbo kubwa kuliko wengine ndiye atakua mshindi na ndiye mwenye mvuto zaidi kwa wanawake na huyo hupewa mke mrembo zaidi.
Kwa ujumla, mila na tamaduni ni sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii yoyote. Ingawa baadhi ya desturi hizi zinaweza kuonekana za kushangaza, za kutisha au hata zisizoeleweka kwa jamii za nje, kwa wenyeji wake huwa ni jambo la kawaida linalojengwa juu ya imani, historia na mtiririko wa maisha ya kila siku. Ni muhimu kukumbuka kuwa tofauti zetu za kiutamaduni hazipaswi kuwa chanzo cha dharau bali fursa ya kujifunza, kuheshimiana na kuenzi utofauti wetu kama Waafrika na wanadamu kwa ujumla.
Related articles;
Cultural centres in East Africa.
https://historyforumtz.blogspot.com/2024/02/cultural-centres-in-east-africa.html
Comments
Post a Comment